Wednesday, May 21, 2008

Mafunzo ya Kujilinda Dhidi ya Ugaidi

Ratatatat!!...Taah!!...Mwenzako chini...Haraka sana unamuwahi pale chini ili upate kumuondoa kutoka katika eneo la hatari...Si ndiyo?..Nyooooo....Tokeza kidogo...Risasi Buuh..kwenye hilo bichwa lako..ubongo wako nduguzo watakuja wataukuta kulee vichakani..Unafikiri hii ni sinema ya seba mwanangulu?..Kwanza inakupasa kulikagua eneo la hatari kabla hujajitokeza..mara nyingi gaidi atamtumia huyo mwenzako aliyejeruhiwa kuwa chambo ili kukunasa pale utakapotaka kumsaidia. Mkakati ni huu; Macho na Mtutu...yaani; mtutu wa silaha yako unaelekea kule macho yako yanapotazama. Ole wako ulete makengeza! Swali; Itazame vizuri hiyo picha,..Unaweza kuniambia adui amejibanza wapi? Unazo sekunde tatu na nusu.....Pia huyo jamaa mwenye blue t-shirt kuna kosa lingine amefanya..lipi?...Sekunde moja.

No comments: